Washika mtutu wa kaskazini mwa jijini London, Arsenal wameripotiwa kuwa tayari kusikiliza ofa kutoka kwenye klabu yoyote duniani, itakayomuhusu kiungo wao kutoka nchini Wales, Aaron Ramsey.

Gazeti la The Daily Mail, limeandika kwamba Arsenal wapo tayari kumuuza kiungo huyo anayependwa na mashabiki wengi wa klabu hiyo, kwa lengo la kutotaka kumuharibia mustakabali wa soka lake.

Taarifa hizo zinaendelea kufafanua kwamba, kuna wasiwasi mkubwa wa Ramsey kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Arsenal, kutokana na mpango ulioandaliwa na meneja Arsene Wenger wa kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Uswiz na klabu ya Granit Xhaka.

Hata hivyo mpaka sasa hakuna klabu yoyote iliyoonyesha nia ya kutaka kumsajili Ramsey ambaye bado ana mkataba wa muda mrefu wa kuitumikia klabu ya Arsenal, lakini inaaminiwa huenda mambo yakaiva itakapofika mwishoni mwa msimu huu, ama baada ya fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016).

Ramsey amekua katika kiwango kizuri kwa muda wa misimu mitatu mfululizo lakini inahofiwa huenda akapoteza makali yake atakapoanza kuwania namba katika kikosi cha kwanza dhidi ya kiungo Xhaka.

Ramsey alisajiliwa na Arsenal mwaka 2008 akitokea Cardiff City, na aliwahi kutolewa kwa mkopo katika vipindi viwili tofauti ambapo katika msimu wa mwaka 2010–2011 alijiunga na Nottingham Forest na sehemu ya mwisho ya msimu huo alisajiliwa na Cardiff City.

Mpaka sasa ameshaitumikia Arsenal katika michezo 182 na kufunga mabao 28.

Maamuzi Ya Mtu Mmoja Yamemuondoa Sinisa Mihajlovic AC Milan
Sakata la Ufisadi wa Mabilioni ya Jeshi la Polisi lageuka kaa la moto