Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal) watalazimika kuvaa jezi ya ugenini katika mchezo wa leo, wa ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaowakutanisha na mabingwa wa soka nchini Uswiz FC Basel, licha ya kuchezwa kwenye uwanja wa Emirates.

Arsenal wameamrishwa kuvaa jezi za ugenini kwa kigezo kilichotumiwa na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA cha kuangalia kufanana kwa jezi za timu zinazokutana bila kujali ni wapi mchezo unapochezewa.

Kanuni hiyo kwa UEFA imepewa jina la “unusual situation (Hali Isio Ya Kawaida)”.

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Arsenal imeeleza kuwa: “UEFA wametuamrisha kuvaa jezi za ugenini katika mchezo wa leo. “Ni hali ambayo haikutarajiwa hivyo hatuna budi kufuata agizo hilo.

“Imebainika jezi za FC Basel zinataka kushabihiana na jezi zetu.

Kitendo hicho kitakua kinawakumbusha mashabiki wa Arsenal ambao kwa mara ya kwanza walikishuhudia kikosi chao kikivaa jezi za ugenini kwenye uwanja wao wa nyumbani msimu wa 1998/99, wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Lens ya nchini Ufaransa.

Jaji Warioba Awaasa Vijana Kuenzi na Kuitunza Amani
Picha 8: Rais Magufuli azindua rasmi ndege mbili mpya za Air Tanzania