Arsenal wameanza mipango ya kulazimisha kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo kutoka nchini Uswiz na klabu ya Borussia Monchengladbach, Granit Xhaka.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka, 23, amekua katika tetesi za usajili wa klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London kwa majuma kadhaa, huku ikielezwa yupo tayari kuondoka nchini Ujerumani na kwenda kusaka changamoto mpya nchini England.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ametenga kiasi cha Pauni million 24, ambacho anaamini kitatoasha kumsajili Xhaka wakati wa majira ya kiangazi ambapo kutakua na purukushani za usajili wa wachezaji kadhaa barani Ulaya.

Hata hivyo mzee huyo kutoka nchini Ufaransa, huenda akapata kipingamizi cha kuhitimisha mpango wa usajili wa Xhaka, kufuatia uongozi wa klabu ya Monchengladbach kutangaza kumuweka sokoni mchezaji huyo kwa Pauni million 32.

Kama mamabo yatakwenda namna Wenger anavyotaka, Xhaka anatarajiwa kuwa mchezaji watatu kusajiliwa kwa kiasi kikubwa cha pesa klabuni hapo, akitanguliwa na Mesut Ozil aliyepelekwa Emirates Stadium kwa ada ya uhamisho wa Pauni million 42.5 mwaka 2013, akifuatiwa na Elexis Sanchez aliyesajiliwa kwa ada ya uhamisho wa Pauni million 32 mwaka uliofuata.

Wenger amedhamiria kumsajili Xhaka, kutokana na hitaji la mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo alilonalo kwa sasa, kufuatia mtihani unaomkabili wa kutarajia kuwaachia akina Mathieu Flamini, Mikel Arteta na Tomas Rosicky mwishoni mwa msimu huu.

Chicharito Athibitisha Ubora Dhidi Ya Washambuliji Wa Man Utd
Ronaldo, Messi Watuhumiwa Kumbana Neymar