Klabu ya Arsenal imempa ofa ya mkataba mpya mshambuliaji wake wa pembeni kutoka nchini England Alex Oxlade-Chamberlain.

Gazeti la The Daily Star limetoka na taarifa zinazoeleza kuwa, Arsenal wamempa mkataba mshambuliaji huyo wa miaka minne ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni 125,000 kwa juma.

Mpango huo umekamilishwa na viongozi wa Arsenal, kutokana na chokochoko zinazoendelezwa na Chelsea dhidi ya mchezaji huyo, ambaye amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja huko kaskazini mwa jijini London.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte, ameonyesha nia ya kutaka kufanya kazi na Chamberlain mwenye umri wa miaka 24, na tayari ameshatenga kiasi cha Pauni milioni 40 ambacho anaamini kitatosha kumuhamishia Stamford Bridge, kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwishoni mwa mwezi huu.

Mkataba wa sasa wa Oxlade-Chamberlain unamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni 100,000 kwa juma, na tayari alikua ameshaanza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Arsenal lakini majuma kadhaa yaliyopita taratibu hizo zilififia.

Rais Magufuli akutana na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA)
William Carvalho Akaribia Kutua London