Bao lililofungwa na beki Ashley Williams katika dakika ya 86, lilizima ndoto za Arsenal za kuondoka kwenye uwanja wa Goodison Park na matokeo ya sare.

Bao hilo liliipa ushindi Everton wa mabao mawili kwa moja, hali ambayo inaifanya Arsenal kukubali kichapo cha pili katika ligi ya nchini England kwa msimu huu wa 2016/17.

Hata hivyo Arsenal, walikua wa kwanza kuliona lango la Everton kupitia kwa mshambuliaji wao kutoka nchini Chile Alexis Sanchez katika dakika ya 20, lakini Seamus Coleman aliisawazishia Everton katika dakika ya 44.

Ushindi huo umeiwezesha Everton kufikisha point 23 na kujikita kwenye nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ya nchini England huku Arsenal wakibaki katika nafasi ya pili kwa kuwa na point 34.

Mchezo mwingine wa ligi ya nchini England uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo ulishuhudia AFC Bournemouth wakiwaadabisha mabingwa watetezi Leicester City kwa kuwafunga bao moja kwa sifuri.

Bao la AFC Bournemouth lilikwamishwa wavuni na Marc Pugh katika dakika ya 34 na kuiwezesha klabu hiyo kukwea hadi katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kwa kufikisha point 21.

Ligi hiyo inaendelea tena hii leo kwa michezo kadhaa kuchezwa.

Middlesbrough Vs Liverpool

Sunderland Vs Chelsea

West Ham United Vs Burnley

Crystal Palace Vs Manchester United

Manchester City Vs Watford

Stoke City Vs Southampton

Tottenham Hotspur Vs Hull City

West Bromwich Albion Vs Swansea City

Lewandowski: Naamini Kwa Pamoja Tutafanikisha Malengo
Video: Kijana aliyeishi maisha ya ajabu, asimulia mazito