Wakala wa mshambuliaji Andrea Belotti wa klabu ya Torino, ameitaka Arsenal kujipanga kikamilifu ili kufanikisha usajili wa mchezaji wake katika kipindi hiki cha mwezi Januari.

Tayari Arsenal wameshatuma ofa ya Euro milion 65, kwa lengo la kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, lakini uongozi wa Torino umeiweka kapuni.

Sergio Lancini, wakala wa mshambuliaji huyo, amesema Arsenal wanapaswa kujifikiria zaidi endapo wanahitaji huduma ya Belotti, na kama watafikia dau linalohitajika huko Stadio Olimpico, hakutakua na kipingamizi cha kukamilisha mpango wao.

Amesema kwa sasa mchezaji wake ana thamani ya Euro milion 100, na kama itakua tofauti na hapo biashara ya kumng’oa nchini Italia haitokuwepo.

“Mbali na Arsenal, kuna klabu nyingi zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili, na uongozi wa Torino FC upo tayari kufanyanao biashara, hivyo kwa Arsenal kama kweli wanahitaji kufanya mkakati wa kumsajili Belotti wajipange kisawa sawa. Lancini aliiambia tovuti na Goal.

Tanzania Yashindwa Kusogea Viwango Vya Ubora Duniani
Yannick Ferreira Carrasco Awanyima Usingizi Atletico Madrid

Comments

comments