Meneja wa Klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa wavumilivu na kudumisha imani na mshkamano baada ya kile alichosema kuwa amesikitishwa na wachezaji wake kwa kucheza kwa kiwango cha chini katika mechi ambayo walipokea kipigo cha goli 4-0 kutoka kwa Liverpool katika ligi kuu ya Uingereza.

Gunners ambayo ilipokea kichapo cha goli nne hapo jana kutoka kwa Majogoo wa Liverpool, hawakuweza kupata nafasi hata moja ya kulishambulia lango la wapinzani wao ambao walionekana kuutawala mchezo huo kitu ambacho kiliwaghadhabisha mashabiki wa timu hiyo.

“Iwapo baadhi ya mashabiki na wafuasi wa Arsenaal wanadhani kuwa mimi ndio tatizo, basi naomba radhi kwamba mimi ndiye tatizo, lakini tunataka mashabiki wetu waendelee kuwa nasi hata baada ya uchezaji mbaya, ninawaomba wawe wavumilivu,” Wenger ameiambia Sky Sports

Aidha,mwishoni mwa msimu uliopita kocha Arsenal Wenger aliingia mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuifundisha Klabu hiyo ili iweze kufikia mafanikio iliyojiwekea katika ligi kuu ya Uingereza licha ya baadhi ya mashabiki kumtaka aondoke.

Hata hivyo, Klabu hiyo ilimaliza nafasi ya tano ligi kuu  msimu uliopita na kumaliza nje ya nafasi za kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 21 ambayo wamekuwa na Wenger.

Video: Jinamizi la uchaguzi mkuu 2015 bado laitesa CCM, Hospitali ya Kairuki yaingia matatizoni
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 28, 2017