Klabu ya Arsenal imechezea kichapo cha goli 3-1 dhidi ya Swansea City katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Liberty Stadium kitu ambacho kimeifanya timu hiyo kuondokana na hatari ya kushuka daraja.

Kosa lililofanywa na mlinda mlango wa Arsenal, Peter Cech lilimpa nafasi, Jordan Ayew kufunga bao na kuwaweka wenyeji kifua mbele.

Aidha, mabao mengine ya Swansea City yalifungwa na Clucas, huku bao pekee la Arsenal likifungwa na Nacho Monreal na kupelekea ushindi wa mabao 3-1

“Nahisi tulikuwa dhaifu sana na tulifanya makosa makubwa. vyema zaidi ni kutozungumzia bao la pili na la tatu,Swansea walikuwa makini sana, wenye nidhamu na hamu ya kutaka kushinda. nasikitika, na naamini kwamba hatukucheza kwa kiwango kizuri naamini hatukuwa na nidhamu ya kutosha,”amesema kocha wa Arsenal Arsene Wenger

Hata hivyo, timu ya Swansea City imejinasua katika hatari ya kushuka daraja baada ya kushinda mechi mbili mfululizo katika uwanja wake wa nyumbani.

 

 

LIVE: JPM akizindua Hati ya kusafiria ya Kielektroniki
500 ya nembo yawafukuzisha kazi walimu watatu