Klabu ya Arsenal imetuma Ofa ya Pauni milioni 60 kwenda Klabu ya Brighton & Hove Albion, wakihitaji huduma ya Kiungo kutoka nchini Ecuador Moises Caicedo.

The Gunners wamewasilisha ofa hiyo, baada ya juma moja kupita wakikamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Leandro Trossard akitokea Brighton & Hove Albion.

Siri ya kutumwa kwa ofa hiyo imefichuliwa na Mwandishi wa Habari Fabrizio Romano, baada ya kuchapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Romano ameandika: “EXCLUSIVE: Arsenal wamewasilisha Ofa ya Pauni Milioni 60 kwa ajili ya kumsajili Moises Caicedo huku ofa ya Klabu ya Chelsea ya Pauni Milioni 55 ikiwekwa kapuni juma lililopita.”

“Mazungumzo ya usajili wa kiungo huyo yanaingia katika hatua muhimu kwa mustakabali wa Caicedo.”

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta hajaficha nia yake ya kutaka kuimarisha safu yake kiungo kabla ya tarehe ya mwisho ya kufungwa kwa Dirisha Dogo itakapofika juma lijayo, huku mchezaji wa kimataifa wa Misri, Mohamed Elneny akiwa nje kutokana na tatizo la goti.”

“Mo ni mchezaji ambaye halalamiki kuhusu chochote lakini tuone”, Arteta alisema alipokuwa akizungumzia Elneny kabla ya mchezo wa Ijumaa dhidi ya Manchester City katika raundi ya nne ya Kombe la FA. “Tunahitaji ulinzi zaidi katika safu ya kati, ikiwa tunaweza.”

“Lakini soko hili ni gumu. ila kama ninavyosema kila mara, jambo muhimu zaidi ni kupata matokeo mazuri na muda wa uwanjani na wachezaji ambao tayari tunao uwanjani ni wazuri sana.”

CCM Iringa yataka Watoto wa kiume kuwekewa ulinzi
Rais Samia asherehekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima