Beki kutoka nchini England na klabu ya Arsenal Calum Chambers leo jumatatu anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya, magharibi mwa jijini London yalipo makao makuu ya klabu ya Fulham.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 23, atafanyiwa vipimo, baada ya klabu ya Arsenal kufikia makubaliano na uongozi wa klabu ya Fulham ya kumuuza kwa mkopo huko Craven Cottage.

Chambers anaondoka Emirates Stadium baada ya kusiani mkataba wa miaka minne mwezi Julai mwaka huu, huku akiwa na matumaini makubwa ya kurejea katika himaya ya washika bundiki msimu ujao, akiwa katika kiwango bora.

Meneja wa Fulham Slavisa Jokanovic, anaamini usajili wa beki huyo utamsaidia katika harakati za kufanikisha malengo ya klabu hiyo msimu ujao, baada ya kufanikiwa kupanda ligi kuu akitokea ligi daraja la kwanza msimu uliopita.

Kutokua na uhakika wa kumtumia beki Alfie Mawson, ndio sababu kubwa kwa meneja huyo kutoka nchini Serbia kumuomba kwa mkopo Chambers, ambaye ana matarajio ya kumtumia katika kikosi chake cha kwanza.

Hata hivyo bado meneja huyo amesisitiza kuhitaji huduma ya beki mwingine katika kikosi chake, na anatarajia kumsajili mchezaji mwingine anaecheza nafasi hiyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Alikua amejipanga kumsajili beki Yerry Mina kutoka FC Barcelona, lakini kukamilika kwa dili la mchezaji huyo kuelekea Everton, kumevuruga mipango yake.

Mina aikataa Man Utd, Kutua Goodison Park
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 6, 2018