Arsenal imetinga nusu fainali ya kombe la Europa kwa jumla ya mabao 6-3 dhidi ya CSKA Moscow licha ya kutoka sare ya 2-2 nchini Urusi.

Kikosi cha Arsene Wenger kilikuwa nyuma ya goli 2-0 na kuwa katika presha kubwa kabla ya Danny Welbeck kupachika goli katika kipindi cha pili.

Aidha, Arsenal ambayo inaongoza kwa mabao katika kinyang’anyiro hicho haikushambulia hata mara moja katika dakika 70 za mwanzo na Laurent Kolscieny alipoteza nafasi ya wazi kabla ya Welbeck kufunga.

Bao la Aaron Ramsey dakika za lala salama liliwavunja moyo CSKA Moscow na kuipatia fursa Arsenal kufuzu katika nusu fainali, hivyo kuungana na Atletico Madrid, Marseille na Salzburg.

Hata hivyo, Kikosi cha Viktor Goncharenko kilikuwa na ndoto ya kuwashangaza Arsenal wakati Chalov alipofunga bao la kwanza.

Amnywesha sumu mwanae kunusuru ndoa yake
Wamiliki wa mitandao ya kijamii watakiwa kujisajili

Comments

comments