Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameliambia jarida la The Sun kuwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ndiye mwanasoka bora duniani.

“Labda Messi,” alisema Mfaransa huyo alipoulizwa anadhani nani anafaa kuwa mchezaji bora.

Messi ni moja ya wachezaji bora wa muda wote, na wengi hukubaliana na Wenger kuwa ndiye mwanasoka bora katika sayari hii kwa sasa.

Mwargentina huyo amerejea siku chache baada ya kuuguza majeraha kwa muda kidogo na ameonyesha uwezo mkubwa bado.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa juu katika soka kwa muda usiopungua miaka 10, umahiri wake unamfanya kuwa tofauti na wachezaji wengine.

Hata hivyo, mwingine ambaye hastahili kusahauliwa ni Cristiano Ronaldo. Ingawa nyota huyo wa zamani wa Manchester United hajawa kwenye kiwango chake cha juu msimu huu, bado anabakia kuwa Mwanasoka tishio na maridadi duniani.

Ronaldo hajaifanyia Real Madrid kazi anayofanya mara zote katika mechi kubwa msimu huu, lakini ukweli ni kwamba kudumu kwake kwenye mbio za kuwania tuzo ya Ballon d’Or kunadhihirisha kuwa bado ni mchezaji mahiri.

Hali kadhalika huwezi kuwaacha nyota wawili wa Barcelona Luis Suarez na Neymar unapojadili mchezaji yupi ni bora duniani.

Nyota wa kimataifa wa Brazili Neymar ni moja ya wachezaji watatu waliopendekezwa kuwania tuzo ya Ballon d’Or, wakati straika wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez ameongeza uwezo wake zaidi ya mara dufu tangu alipotua Barcelona msimu wa majira ya joto 2014

Justice Majabvi Kuchagua Mbivu Ama Mbichi Za Simba
Mjumbe Wa Kamati Ya Utendaji Yanga Afunika Kombe