Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal), wanajipanga kuushtua ulimwengu kwa kuwasilisha ofa ya usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast pamoja na klabu ya Manchester City, Wilfried Bony.

Gazeti la The Daily Star limeripoti kuwa, meneja wa Arsenal Arsene Wenger anajiandaa kuwasilisha ofa ya Pauni milioni 30 ambayo anaamini itatosha kumng’oa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 huko Etihad Stadium.

Arsenal wamepewa nguvu wa kufikiria jambo hilo, baada ya kupata uhakika wa mipango ya meneja wa Man City, Pep Guardiola ambayo haimpi nafasi Bony ya kucheza mara kwa mara kutokana na ujio wa mshambuliaji kutoka nchini Hispania Manuel Agudo Durán “Nolito”ambaye atakua akisaidiana na Kun Aguero.

Endapo suala la kuuzwa kwa Bonny litapewa baraka na meneja huyo mpya kutoka nchini Hispania, litainufaisha Man City kwa kupata faida ya Pauni milioni 5, kufuatia usajili wa mshambuliaji huyo kuigharimu klabu hiyo kiasi cha Pauni milion 25 mwezi januari mwaka 2015 alipotoka Swansea City.

Frank de Boer: Nitarejeshea Heshima Inter Milan
Olympic 2016 Yawaunganisha Korea Kusini Na Kaskazini