Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal), wametenga kiasi cha Pauni million 34, kwa ajili ya usajili wa kiungo kutoka nchini Uswiz pamoja na klabu ya Borussia Monchengladbach ya nchini Ujerumani, Granit Xhaka.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amehusishwa kwa muda mrefu na taratibu za usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, na kwa sasa anaamini huenda akampata kutokana na fungu la pesa alilolitenga.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la The Sun la nchini England, umebaini kwamba, meneja huyo kutoka nchini Ufaransa amedhamiria kumsajili kiungo huyo kabla ya kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Uswiz, ambacho kitaelekea nchini Ufaransa kushiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016).

Nguvu ya usajili wa Granit Xhaka, inahisiwa kuongezeka miongoni mwa maafisa wa Arsenal wakiongozwa wa Arsene Wenger, kufuatia uongozi wa klabu ya Borussia Monchengladbach, kushindwa kumshawishi abaki kwa kipindi kingine.

Hata hivyo hapo awali ada ya uhamisho wa Xhaka, ilitajwa kuwa Pauni million19.7, lakini kutokana na uwepo wa klabu kadhaa ambazo zinaiwania saini yake, mchezaji huyo amepandishwa thamani na kufikia zaidi ya Pauni million 25.

Arsene wenger amejipanga kuiboresha safu yake ya kiungo, kufuatia baadhi ya wachezaji wake waliopo kikosini kwa sasa wanaocheza nafasi hiyo kumaliza mikataba yao kama Mathew Flamini, Tomas Rosicky pamoja na Mikael Arteta.

Sakata La Kushuka Daraja, Coastal Union Wainyooshea Kidole TFF
Joe Ledley Kuzikosa Fainali Za Ulaya (Euro 2016)