Aliyekua meneja wa klabu ya Arsenal kwa muda wa miaka 22 Arsene Wenger, ameripotiwa kufanya mazungumzo na uongozi wa AC Milan, kwa ajili ya kuchukua nafasi ya meneja wa sasa wa The Rossoneri Gennaro Gattuso.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na jarida la France Football, Wenger mwenye umri wa miaka 69, anapewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo, na huenda akaanza kazi January 2019.

Uongozi wa AC Milan umemfikiria babu huyo kutoka nchini Ufaransa, kutokana na mwenendo wake wa ukufunzi wa soka, na wanaamini endapo watafikia makubaliano, kuna hatua kubwa huenda wakaipiga katika kufanikiwa kikosi chao kinacheza soka la ushindani.

Kwa sasa kikosi cha AC Milan hakifanyi vizuri kwenye mshike mshike wa ligi kuu ya soka nchini Italia, kama ilivyokua inatarajiwa na uongozi mwanzoni mwa msimu huu, hali ambayo inamuweka mwenye mazingira mabaya meneja Gennaro Gattuso.

AC Milan inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ya Serie A, huku ikiachwa kwa alama kumi na vinara Juventus, ambao pia ni mabingwa watetezi.

Lengo kuu la muwekezaji wa klabu ya AC Milan (US investment fund ElliotManagement Corporation), ni kutaka kuiona klabu hiyo ikifanikiwa kurejea kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao, na tayari imeanza kuaminiwa kuwa, nafasi hiyo huenda isipatikane mwishoni mwa msimu huu, endapo wataendelea kuwa na meneja Gattuso.

Gattuso mwenye umri wa miaka 40, alikabidhiwa kikosi cha AC Milan Novemba 2017, na msimu uliopita alionyesha ukakamavu mzuri kwa kuiongoza klabu hiyo, japo hakufanikiwa kufikia lengo la kuipeleka kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mkataba wa meneja huyo raia wa Italia, unatarajia kufikia kikomo mwei April mwaka 2021.

Sanamu ya Salah yazua gumzo nchini Misri
Kidole cha mke wake champeleka jela maisha