Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameomba radhi kufuatia kitendo chake cha kumsukuma mwamuzi wa akiba Anthony Taylor baada ya mchezo wa jana dhidi ya Burnley, uliochezwa katika uwanja wa Emirates.

Wenger amefanya hivyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu, kusudio la kufanya maamuzi ya kumsukuma mwamuzi huyo, huku akionekana ni mwenye hasira.

Wenger alisema ilitokea kama ajali na wala hakudhamiria, hivyo ni vyema akasamehewa kwa jambo hilo ambalo amekiri sio la kiungwana.

Hata hivyo imedai kuwa, malumbano ya meneja huyo kutoka nchini Ufaransa na mwamuzi Anthony Taylor yaliibuka kufuatia utata wa penati iliyowapatia Burnley bao la kufutia machozi, ambayo ilifungwa na Andre Gray dakika ya 90.

Kuhusu utata wa panati hiyo, Wenger aliwaambia waandishi wa habari haikua sahihi kwa mwamuzi kuamuru mkwaju huo upigwe kwa sababu kulikua hakuna kosa.

“Sikuona uhalali wa panati ile, japo na sisi tulipata penati dakika kadhaa zilizofuata, lakini kwa upande wa wenzetu walizawadia.” Alisema Wenger.

Kwa upande wa meneja wa Burnley Sean Dyche, naye hakuwa mwenye furaha baada ya kikosi chake kutoka uwanjani kikiwa kimekubali kufungwa mabao mawili kwa moja.

Bao la pili la Arsenal lililofungwa kwa mkwaju wa panati na mshambuliaji kutoka nchini Chile, Alexis Sanchez ndio lilikua sababu ya kumnyima raha meneja huyo pamoja na wachezaji wake.

Beki wa Burnley Ben Mee alinyoosha mguu alipokua katika harakati za kuokoa mpira, lakini alijikuta akimpiga usoni beki wa Arsenal Laurent Koscielny, na mwamuzi aliamuru mkwaju wa penati upigwe.

“Ulikua mchezo mgumu hadi mwisho,” Alisema Dyche. “lakini kupoteza point tatu kwa aina hii, haikua sawa hata kidogo.

“Hatukutaka kuwa watukutu ili kila mmoja alione hilo, lakini yoyote aliyefuatilia mchezo ameona ni vipi mambo yalivyoharibiwa kwa maamuzi mabovu.”

Crew Marekani kumshtaki Trump, adaiwa kukiuka sheria
Yaya Toure: Andre Marriner Hakututendea Haki