Mameneja wa klabu za Arsenal na AFC Bournemouth, Arsene Wenger na Eddie Howe wanatajwa kuwa kwenye orodha ya mwisho ya makocha wanaofikiriwa kurithi mikoba ya Sam Allardyce aliyetangaza kujizuzulu kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo.

FA wapo katika mchakato wa kumsaka kocha mpya ambaye atakua na jukumu la kukiongoza kikosi cha Uingereza katika harakati za kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

Gareth Southgate, ametangazwa kuwa kocha mkuu wa muda wa kikosi cha Uingereza ambacho mwishoni mwa juma lijalo kitaendelea na kampeni ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya timu ya Malta.

Gazeti la Daily Mirror limefichua orodha hiyo ya makocha watatu ambao wanapigiwa upatu wa kuchukua nafasi ya kuwa kocha mkuu wa kikosi cha Simba watatu lakini bado jina moja halikutajwa na gazeti hilo.

Wenger na Howe kwa pamoja waliwahi kutajwa kwenye orodha iliyopendekezwa na FA, baada ya kujiuzulu kwa Roy Hodgson miezi minne iliyopita, lakini Allardyce aliwazidi kete na kutangazwa kuwa kocha mkuu.

Hata hivyo inadaiwa kwamba FA huenda wakawa na malengo ya kumpa nafasi Arsene Wenger ya kuwa kocha mkuu wa kikosi cha Uingereza, lakini itawalazimu kusubiri hadi mwishoni mwa msimu huu ambapo mkataba wake na klabu ya Arsenal utakua unafikia tamati.

Lakini pamoja na kuwepo kwa tetesi hizo, bado Howe anaonekana kuwa mpinzani mkubwa wa babu huyo kutoka nchini Ufaransa.

Ancelotti: Juventus Wamelamba Dume Kwa Gonzalo Higuain
Twaweza: Asilimia 60 wanaunga mkono zuio la mikutano ya vyama vya siasa