Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu usajili wa kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Juventus FC, Paul Pogba.

Wenger ambaye anasifika kwa kubana fedha ya usajili pale linapojitokeza suala la mchezaji anaetaka kusajiliwa na klabu ya Arsenal, amesema sio jambo la kawaida kwa Pogba kuwekewa fedha nyingi kama Pauni milion 100.

Wenger alilazimika kuzungumza suala hilo, dakika chache kabla ya kikosi chake hakijaanza mpambano wa kirafiki dhidi ya Chivas Guadalajara mapema leo asubuhi.

Meneja huyo aliyekaa kwa kipindi kirefu katika ligi ya nchini England akiwa na klabu moja, ameufananisha usajili wa Pogba na matumizi mabovu ya fedha.

“Ni suala la ajabu kama huwezi kulipa kiasi hicho. Lakini kama unaweza kulipa unaweza kutolea uchanganuzi. Ni suala la kustaajabisha hasa ukifafananisha na maisha ya kawaida. Huo ndiyo ukweli halisi. Lakini tunaishi kwenye ulimwengu ambao kila shughuli ambayo inahusisha ulimwengu kwa ujumla ina pesa nyingi sana.  Mchezo wa soka umekuwa una ushindani ulimwenguni kote na ndiyo maana vilabu mbalimbali vnaweza kufanya hivyo.”

“Inaweza kuingia akilini mwako kwamba mchezaji anaweza kurudisha pesa zote hizo? Hakuna anayeweza kukokotoa hilo. Na kwasababu ni niko katika tasnia hii, mara nyingine nimekuwa nikifikiri kwamba rekodi haiwezi kwenda mbali kiasi hiko lakini kumbe sikuwa sahihi. Pengine miaka michache ijayo itakuwa 200, 300, nani anajua hilo?” Alisema Wenger.

Paul Pogba anatarajiwa kusaini mkataba wa kiutumikia Manchester United  siku kadhaa zijazo, baada ya kuwa tetesi kwa kmuda mrefu.

Video: Mkia wangu uko pale pale - James Lembeli
Lembeli achungulia CCM, Magufuli aahidi kutomkata 'mkia' akirudi