Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amewatumia salamu mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona kuhusu uwezekano wa kumruhusu beki wa pembeni Hector Bellerin kurudi Camp Nou.

Wenger ametuma salamu hizo, alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo The Gunners watapambana na Swansea City katika uwanja wa Emirates.

Wenger amesema ni vigumu kukubali kumuachia beki huyo ambaye alimsajili akiwa na umri wa miaka 16 kama sehemu ya makubaliano ya kumuuza aliyekua kiungo na nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas mwaka 2011.

Makamu wa rais wa FC Barcelona Jordi Mestre amewahi kukaririwa na vyombo vya habri vya nchini Hispania akieleza mpango wa kumrejesha Bellerin Camp Nou kufuatia kikosi chao kukabiliwa na changamoto ya beki wa kulia, baada ya kuondoka kwa Dani Alves aliyetimkia Juventus FC.

Nike Yavunja Mkataba Wa Adidas, Kuidhamini Chelsea Hadi 2032
Video: Makonda atimiza ahadi yake kwa kijana aliyetobolewa macho na Scorpion, kununuliwa nyumba, pikipiki 5 na bajaji 2