Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger anaendelea kuumiza kichwa kuhusu kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil ambaye bado hajathibitisha kama atasaini mpkata mpya.

Wenger amekua katika mpango wa mazungumzo na mchezaji huyo aliyemsajili mwaka 2014 akitokea kwa mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid, ambao walikubali kumuachia kwa kitita cha Pauni milioni 42.4.

Mkataba wa sasa wa Ozil unatarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao ambao unamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni laki mbili (200,000) kwa juma.

Meneja huyo kutoka nchini Ufaransa anaamini Ozil atakubali kusaini mkataba mpya ili aweze kuwa sehemu ya kikosi chake kwa miaka kadhaa ijayo kwa malengo ya kusaka mafanikio.

Hata hivyo mzee huyo mwenye umri wa miaka 66, amekanusha taarifa za mpango wake wa kumsainisha mkataba mpya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, kukwamishwa na suala la fedha ambazo zitatumika kama mshahara wake kwa juma.

“Sina imani na hilo linalozungumzwa kwa sababu namfahamu vizuri Ozil, sio mtu ambaye ameweka mbele suala la fedha bali anachokihitaji katika maisha yake ni kucheza soka kwanza na mengine ndio yafuate,

“Jambo la kusaini mkataba mpya halihitaji nguvu ya ziada ya kumbembeleza, bali kinachofanyika sasa ni kuangalia namna ya kulimaliza suala hili ili mambo mengine yaendelee.

“Anataka kuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kwa kipindi kingine. Na Nina uhakika tutalifanikisha suala hilo. Alisema Wenger

Arsenal kwa sasa inaendelea na mpango wa kuwasainisha mikataba mpya baadhi ya wachezaji ili kuziba mianya ambayo huenda ikatumiwa na wapinzani wakati wa dirisha dogo la usajili ama itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Watzke: Real Madrid Wanakaribishwa Kwa Mazungumzo
Jose Mourinho Afunguka Kuhusu Mwamuzi Anthon Taylor