Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemkana kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya West Ham Utd Dimitri Payet.

Wenger amemkana kiungo huyo, baada ya kuhusishwa na taarifa za kuwindwa na washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal), katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Mzee huyo kutoka nchini Ufaransa alikanusha taarifa za kuwa katika mpango wa kumsajili payet, alipokutana na waandishi wa habari jana katika mkutano maalum uliokua unazungumzia mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England wa mwishoni mwa juma hili, ambapo The Gunners watapapatuana na Burnley.

“Binafsi ni mshabiki mkubwa wa Payet kutokana na uwezo wake mzuri wa kucheza soka, lakini sina mpango wa kumsajili kama ilivyoripotiwa na baadhi ya waandishi wa habari ambao naamini ni miongoni mwenu,” Alisema Wenger.

“Tuna wachezaji wengi ambao wana uwezo wa kucheza kama Payet, hivyo hakuna sababu ya kumsajili kwa sasa.”

Payet amekua kwenye shinikizo la kutaka auzwe katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, na juma lililopita aligomea mazoezi, hali ambayo ilisababisha aondolewe kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Crystal Palace.

Video: Waziri Nape aeleza kusikitishwa na shutuma kuhusu bidhaa feki za wasanii
Kafulila: Chadema hii ni ya mwendo kasi