Meneja wa Washika Bunduki wa Kaskazini mwa jijini London *Arsenal*, Mikel Arteta amesema klabu yake inatakiwa kuiga utamaduni wa kushinda ambao wamekuwa nao wapinzani wao Chelsea katika miaka 15 iliyopita.

Chelsea imetwaa mataji 16 tangu Roman Abramovich alipofanya uwekezaji kwenye klabu hiyo 2003. Hakuna timu nyingine ya Kiingereza ambayo inaweza kulinganishwa na Chelsea tangu wakati huo.

Meneja wa sasa wa Chelsea, Frank Lampard ambaye atakabiliana na Arteta leo Jumamosi kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la FA utakaopigwa Uwanja wa  Wembley mishale ya saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ni meneja wa 12 chini ya utawala wa  Abramovich.

“Wao (Chelsea) walikuwa na wachezaji muhimu sana kwenye vikosi vyao vilivyoshinda na labda imewapa nguvu ya kuwa thabiti.

“Wamesimamiwa na makocha wazuri. Kabla ya Abramovich, hawakuwa timu ya kushinda. Lakini walifanikiwa kubadilisha mawazo na kuwashawishi wachezaji na kuweka shinikizo kwa kila mtu kwenye klabu kwamba lengo pekee  kwao ni kushinda.”

“Mambo yakiwa hivyo unakuta kila mmoja anafanya vizuri,” amesema.

Arsenal wataingia na presha kwenye mchezo wa leo kutokana na wenzao Chelsea kuwa tayari na nafasi ya kushiriki msimu ujao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ushindi kwa Arsenal katika mchezo wa leo mbali na ubingwa utawapa ticketi ya kucheza Europa Ligi msimu ujao.

Kama watapoteza inaama kuwa Arsenal watapoteza nafasi ya kushiriki michuano hiyo ya Ulaya kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 25 hivyo itabidi watumia nguvu kubwa kuwazuia kuondoka baadhi ya wachezaji wao ambao kila msimu wamekuwa na kiu ya kucheza michuano hiyo.

Tuchel afunga ukarasa wa Ufaransa kwa furaha
NEC yatoa maelekezo kwa wasimamizi Uchaguzi mkuu