Mchungaji ambaye jina lake limehifadhiwa, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa tuhuma za kumbaka muumini wake wakati anamuombea apone maradhi nyumbani kwake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuf Ilembo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea Juni 3 mwaka huu mkoani humo.

Kaimu Kamanda Ilembo alieleza kuwa mchungaji huyo alimuomba muumini wake afike nyumbani kwake ili amfanyie maombi kutokana na maradhi yanayomkabili kwa madai kuwa alikuwa amelishwa sumu, lakini alipofika nyumbani ambapo mkewe alikuwa amesafiri, mchungaji huyo alibadili zoezi na kumbaka.

Alieleza kuwa Juni 10 mwaka huu, msichana huyo akiwa nyumbani kwao, dada yake aliona ujumbe kwenye simu yake kutoka kwa mchungaji huyo akimuomba radhi kwa kile alichomfanyia akitaka asimwambie mtu yoyote, ndipo alipoanza kumdadisi na kutaka maelezo ya kina.

Kamanda Ilembo alisema kuwa baada ya msichana huyo kuridhia na kumsimulia tukio hilo la ubakaji, dada yake aliongozana naye na kutoa taarifa kituo cha polisi, taarifa zilizopelekea kukamatwa kwa mchungaji huyo.

Kutokana na maradhi yanayomkabili msichana huyo na tukio hilo la ubakaji, alipewa fomu namba tatu kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu.

Magaidi wa ISIS watajwa mauaji ya watu 50 Marekani
Video: Mbowe akamatwa, Zitto asakwa. Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bil. 2