Makamu wa rais wa klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa, Vadim Vasilyev amesema mshambuliaji kutoka nchini Colombia, Radamel Falcao atarejea klabuni hapo akitokea Chelsea alipokua akicheza soka kwa mkopo.

Falcao aliakua hana msimu mzuri tangu aliposajiliwa na klabu ya Chelsea mwezi Julai mwaka 2015 kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja, na ilimuuwia vigumu kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Vasilyev amesema mshambuliaji huyo atarejea nchini Ufaransa, kutokana na mipango yao kushindwa kufanikiwa ya kumuuza moja kwa moja endapo angeonyesha kiwango kizuri akiwa na Chelsea.

Hata hivyo Vasilyev anaamini Falcao bado ana uwezo wa kucheza soka na kuihangaisha safu ya ulinzi ya timu yoyote pinzani, lakini akasisitiza jambo hilo litafanikiwa baada ya benchi lao la ufundi kufanya kazi ya ziada ya kumrejeshea makali yake, sambamba na kujituma kwake mazoezini.

“Bado tuna matumaini na Falcao kwa kuamini ana uwezo mkubwa wa kucheza soka, na ninakuhakikishia hana muda mrefu atarejea katika kiwango chake.”

“Wakati mwingine hutokea kama bahati mbaya kwa wachezaji, hivyo hatukushangazwa na uwezo wa Falcao kushuka kwa kiasi kikubwa na ndio maana tumeamua kumrejesha kundini kwa ajili ya kumjenga upya,” alisema Vasilyev.

Klabla ya kujiunga na Chelsea, Falcao alisajiliwa kwa mkopo na klabu ya Man Utd katika msimu wa 2014-15, lakini kiwango chake kilikua kikwazo kuendelea kuwepo Old Trafford ambapo pia waliweka mikakati ya kumsajili moja kwa moja kama angewaridhisha.

Rais Wa Inter Milan Ampigia Magoti Roberto Mancini
Zlatan Ibrahimovic Aingia Kwenye Rada Za SSC Napoli