Kiungo kutoka nchini Ureno, Joao Moutinho huenda akajiunga na washika bunduki wa Ashburton Grove, Arsenal kufuatia uongozi wa klabu ya AS Monaco kumpa ruhusa ya kufanya hivyo.

Arsenal wanamsaka mrithi sahihi wa kiungo kutoka nchini Ufaransa, Mathieu Flamini ambaye yu mbioni kuuzwa nchini Uturuki kwenye klabu ya Galatasaray.

Uongozi wa AS Monaco umefikia maamuzi ya kumpa ruhusa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 kuondoka, kufuatia hali yao kiuchumi kutokau nzuri kwa sasa, hivyo wanahitaji kupunguza matumizi.

Ada ya usajili ya Moutinho, imeshatajwa kuwa ni paund million 14 na atakapoondoka klabuni hapo atapunguza matumizi ya fedha ambazo zilikua zikilipwa kama mshahara wake kwa juma ambao ni paund 110,000.
Wakati Arsenal wakipewa nafasi kubwa ya kumsajili Moutinho, klabu ya Zenit St Petersburg ya nchini Urusi pamoja na FC Porto ya nchini Ureno, zinatajwa kuwa katika kinyang’anyiro hicho.

Ni Vita Kati Ya Benitez, Van Gaal Na Ramos
Kenyatta Amgomea Obama Kuhusu Ushoga