Mabingwa wa soka nchini Ufaransa AS Monaco wametangaza kumsajili kiungo mkabaji wa Lille, Soualiho Meite kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 8.

Meite mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na AS Monaco kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kufanyiwa na kufaulu vipimo vya afya.

AS Monaco wamemsajili Meite baada ya kuvutiwa na kiwango alichokionyesha msimu uliopita, wakati alipokuwa akiitumikia Zulte Waregem ya Ubelgiji kwa mkopo.

Image result for Soualiho Meite to AS MonacoPicha ya kumkaribisha Soualiho Meite AS Monaco.

Akiwa na Zulte Waregem, Meite aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa kombe la Ubelgiji. Akicheza michezo 30 na kufunga bao moja huku akitengeneza bao moja.

Méité anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na AS Monaco tangu kufungulia kwa dirisha la usajili mapema mwezi huu. Wengine ni Diego Benaglio,Jordy Gaspar na Youri Tielemans.

Waraka Wa Zito Kabwe Kwa Wadau Wa Soka
Serikali yang'ata na kupuliza, yasema haitavichukulia hatua vyombo vya habari vinavyoikosoa