Klabu ya AS Roma ya nchini Italia bado haijakata tamaa ya kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Algeria Riyad Mahrez.

Mkurugenzi wa michezo wa AS Roma Monchi amesema bado wana matumaini makubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa klabu ya Leicester City, ambayo msimu uliopita iliupoteza ubingwa wa England.

Monchi amekaririwa na baadhi ya vyombo vya habari vya England akisema, wataendelea kujaribu bila kuchoka katika suala hilo, na wanaamini kabla ya dirisha kufungwa mwishoni mwa mwezi huu watakua wamepata jibu sahihi la kumpata Mahrez ama kumkosa.

“Binafsi ninafurahishwa na kasi ya klabu katika suala la kuisaka saini ya Mahrez, nimekua na mchango mikubwa sana katika hili, tunaamini ofa yetu ya Euro milioni 30 tunayotarajia kuituma wakati wowote juma hili huenda ikakubaliwa.” Monchi aliviambia baadhi ya vyombo vya habari vya England.

“Kama kumbukumbu zangu zitakua sahihi, jaribio hili litakua la tatu kwetu, lakini ninaendelea kusisitiza hatutochoka katika suala la kumsajili Mahrez, kwa sababu tunaamini ni mchezaji mzuri ambaye atatufaa kwenye msimu mpya wa ligi ya Sirie A.”

“Tunashukuru kuona mchezaji mwenyewe ameshaonyesha nia ya kutaka kuondoka King Power Stadium, na kilichobaki kwa sasa ni msimamo wa viongozi wake kugoma kumuachia.”

Mahrez, aliutaarifu uongozi wa Leicester City kuwa anataka kuondoka, baada ya kuona lengo lililokua limewekwa klabuni hapo msimu uliopita la kutetea taji kushindwa kutimizwa kikamilifu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ameshaifungia Leicester City mabao 35 katika michezo 100 aliyocheza tangu aliposajiliwa mwaka 2014 akitokea Le Havre ya nchini Ufaransa.

Alexis Sanchez Kuzikosa Leicester City, Stoke City
Hizi Ndio Sababu Za Ngassa Kukwama Kwenye Usajili Wa Young Africans