Klabu ya AS Roma imekua ya kwanza kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kwa mkopo kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere lakini imeutaka uongozi wa The Gunners kukubali kuchangia sehemu ya fedha za mshahara wake.

Aliyekua mkurugenzi wa soka wa klabu ya Tottenham Hotspur Franco Baldini, ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya AS Roma amethibitisha mipango ya kutaka kumsajili Wilshere baada ya kuushawishi uongozi wake kufanya hivyo kutokana na kumfahamu vizuri kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.

Taarifa nyingine kutoka nchini Italia zinadai kuwa, mabingwa wa soka nchini humo Juventus FC nao wapo katika harakati za kutaka kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumuwania Wilshere.

Kwa upande wa England klabu ya West Ham nayo imetajwa kuwa kwenye heka heka wa kutaka kutuma ofa ya kumsajili kwa mkopo.

Wayne Rooney Kustaafu Soka Mwaka 2018
Ndege za kijeshi kuruka anga la Dar Septemba 1