Klabu ya Man City huenda ikaingia mtegoni kufuatia mipango iliyoandaliwa na uongozi wa AS Roma wa kutaka kutuma ofa ya usajili wa wachezaji watatu Pablo Zabaleta, Bacary Sagna pamoja na Gael Clichy.

AS Roma wamejipanga kukamilisha mchakato huo itakapofika mwezi januari mwaka 2017 wakati wa usajili wa majira ya baridi (Dirisha dogo) kwa kuamini katika kipindi hicho itakua ni rahisi kwao kuhitimisha wanalolihitaji.

Wachezaji hao wanatarajia kumaliza mikataba yao ya kuitumikia Man City itakapofika mwishoni mwa msimu huu, na inaaminika haitokua rahisi kwa uongozi wa Man City kuwaruhusu kuondoka Ethiad Stadium wakiwa huru.

Image result for Pablo Zabaleta, Bacary Sagna and Gael Clichy Bacary Sagna, Pablo Zabaleta pamoja na Gael Clichy

AS Roma kwa sasa wanakabiliwa na tatizo kubwa katika safu yao ya ulinzi na wanaamini wachezaji hao kama watafanikiwa kuwasajili mwezi januari mwaka ujao, watakuwa wamemalizana na changamoto hiyo.

Selfie Za Wachezaji Wa Arsenal Zawakera Magwiji
Wachina Kumrudisha Big Sam Stadium Of Light