Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limepanga Ratiba ya Hatua ya 64 ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ msimu huu 2022/23, ambayo itaanza kuchezwa kati ya Desemba 09-11.

Bingwa Mtetezi wa Michuano hiyo Young Africans amepangwa kucheza nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Kurugenzi FC ya Mkoani Simiyu inayoshiriki Ligi Daraja la Pili ‘First League’.

Simba SC iliyotwaa ubingwa wa ‘ASFC’ msimu wa 2019/20 na 2020/21 imepangwa kuanza safari ya kusaka ubingwa wa Michuano hiyo msimu huu kwa kucheza na Eagle FC ambao ni wanashiriki Ligi ya Mabingwa wa mkoa, mchezo utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.

Meneja wa mashindano TFF, Baraka Kizuguto amesema michezo hiyo ya Hatua ya 64 itachezwa kwa kuangaliwa utaratibu wa kupishana viwanja, kuepusha ratiba kuingiliana.

“Umeona tuna tarehe 9 na 11 kwa hiyo kati ya hapo timu lazima zipishane kucheza, bingwa wa Mashindano haya ndio atakata tiketi ya kushiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afriak msimu ujao wa 2023/24.” amesema Kizuguto.

Michezo mingine ya Hatua ya 64 Kombe la ‘ASFC’

Geita Gold vs Transit Camp (Nyankumbu, Geita)
Ihefu vs Mtama Boy (Highland State)
Kagera Sugar vs Buhare FC (Kaitaba)
Dodoma Jiji vs TMA Stars (Jamhuri,Dodoma)
Ruvu Shooting vs Ndanda (Uhuru)
Namungo vs Kitayosce (Majaliwa)
Polisi Tz vs Nyika FC (Ushirika)
Mbeya City vs Stand Fc (Sokoine)
Mtibwa Sugar vs TRA (Manungu)
Prisons vs Misitu (Sokoine)
Singida Bs vs Lipuli FC (Liti)
Coastal Union vs Tanga Middle (Mkwakwani)
KMC VS Tunduru (Uhuru)
Azam vs Malimao (Chamazi)
Fountain Gate vs Rhino Rangers (Jamhuri, Dodoma)
JKT Tanzania vs Biashara Utd (Mej G. Isamuhyo)
Nduguti Stars vs Gwambina (Liti)
African Lyon vs Mbuni (Uhuru)
Kigoma Kwanza vs Buhaya (Lake Tanganyika)
Cosmo Politana vs Mbeya Kwanza (Uhuru)
Majimaji vs Ken Gold (Lake Tanganyika)
Mashujaa vs Pamba (Lake Tanganyika)
Polis Katavi vs Mbeya Road
Mbao Fc vs Mapinduzi Fc (Nyamagana)
Green Warriors vs Stand Utd (Mej G. Isamuhyo)
Silent Ocean vs Copco (Uwanja utapangwa)
Magereza DSM vs Pan African (Uhuru)
E4M vs New Dundee (Samora)
Afya FC vs African Sports (Uwanja utapangwa)
Nzega vs KFC Fc

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Decemba 2022
Ihefu FC kusajili wawili Dirisha Dogo