Mkurugenzi na mmliki wa bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini Twanga Pepeta, Asha Baraka amedai yupo mbioni kuachana na maswala ya muziki na kujikita kwenye siasa. Hivyo alizisihi media zisiwe na upendeleo katika kupiga muziki kwani media nyingi hazipigi muziki wa bendi kwa uwiano  sawa na nyimbo nyingine.

“Muziki unakuwa kwa kasi sana japo kuwa bado kuna changamoto nyingi kama unavyojua, media nyingi hazipigi nyimbo za muziki wa bendi kwa uwiano sawa na nyimbo za aina zingine za muziki. Kwa hiyo media zibadilike kwa sababu sisi wengine tunajipanga kuwaachia vijana na kuingia kwenye siasa,” Asha Baraka alizungumza hayo alipohojiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV.

Asha Baraka amedai tayari ameshafanya kazi kubwa kwenye muziki wa dansi na muda huu ni kwa ajili ya vijana na yeye aingie kwenye siasa.

Pia alisema anaamini wizara yenye dhamana na maswala ya burudani itafanya juhudi za kusaidia kuurudisha muziki wa dansi katika chati kwa mwaka 2017.

Serikali kuajiri walimu 4000 wa masomo ya sayansi na hisabati
Machali: JPM aongeze kasi ya utumbuaji majipu