Mkali wa RnB, Ashanti amefunguka kuhusu kejeli alizorushiwa na 50 Cent baada ya tamasha lake lililokuwa limepangwa kufanyika katika chuo kimoja nchini Marekani kuuza tiketi 24 tu.

Waandaaji wa tamasha hilo walitangaza kuahirisha wakieleza kuwa muitikio umekuwa mdogo kuliko walivyotarajia hivyo wameamua kuachana nalo.

Kufuatia hatua hiyo, Curtis Jackson (50 Cent) alitumia mtandao wa Instagram kumkejeli Ashanti akidai kuwa amekuwa akimshauri aache kuwa karibu na Ja Rule ili aweze kufanikiwa.

50 Cent na Ja Rule wamekuwa na uhasama wa kimuziki wa muda mrefu, kiasi cha kumfanya kiongozi huyo wa G-Unit kuanza kumuandama pia Ashanti ambaye ni mshirika mkubwa na wa muda mrefu wa hasimu wake huyo.

Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano na TMZ, Ashanti alisema kuwa 50 Cent alijitoa akili na kwamba siku zote amekuwa mtu wa kuwanyanyasa watu.

“Afisa Curtis anajitoa akili,” alisema Ashanti. “Ilikuwa kawaida na waandaaji walieleza wazi kuwa sababu ilikuwa ni kutokuwepo kwa matangazo ya kutosha kuhusu tamasha langu,” aliongeza.

Hata hivyo, 50 Cent amefuta ‘post’ zake kuhusu Ashanti na hivi sasa amejikita katika kutangaza ujio wa msimu wa sita wa show yake maarufu ya runinga ya ‘Power’.

Utetezi wa Amber Rutty akijisalimisha polisi kuhusu video chafu
Lugola ajibu kuhusu waliomteka Mo Dewji, ‘mnaulizia Mo tu..!’

Comments

comments