Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro, linamshikilia mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Yahya Idd mkazi wa Njoro kwa tuhuma za kubaka na kulawiti watoto 5, wanaosoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Chemchem, iliyopo Manispaa ya Moshi.

Hayo yamesemwa na kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamis Issah ambapo amesema kuwa tukio hilo limetokea Julai 15, baada ya watoto hao wenye umri kati ya miaka nane na kumi, kufanyiwa ukatili huo wakati wa mapumziko.

Kwa mujibu wa kamanda imeelezwa kuwa, watoto hao walitoroka shuleni na baada ya kurejea, mmoja wa wale watoto alikuwa anatembea huku akichechemea na baada ya kuhojiwa walidai wametoka kwa babu Yahya.

Na kwamba uchunguzi wa awali, umeonyesha watoto hao kubakwa, huku mmoja akiwa amelawatiwa.

Skimu za umwagiliaji zapaisha uchumi wa Mvomero
TCU yaanza usajili wanafunzi elimu ya juu