Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Mazengo Chati kwa kumlawiti mama yake mzazi akiwa hajitambui, katika Kijiji cha Manchali wilayani Chamwino, jambo ambalo ni kinyume kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi jijini Dodoma, Gilles Muroto alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa kijana Mazengo Chati mwenye umri wa miaka 28, amembaka mama yake mzazi mwenye miaka 56 na ametenda kosa hilo kwa madai ya ulevi pamoja na imani za kishirikina.

“Tukio la kijana Mazengo limetokea katika Kijiji cha Manchali ambapo kijana huyo alimlawiti mama yake mzazi akiwa hajitambui, na kwa sasa tunamshikilia kwa ajili ya kumfikishwa mahakamani,”amesema kamanda Muroto

Katika hatua nyingine, kamanda Muroto amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wengine wawili, kwa makosa ya ulawiti na ubakaji wa watoto na wazee huku mtuhumiwa mmoja akiuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kukutwa akiwa anambaka mwanafunzi wa miaka nane.

 

Uingereza, China zanyosheana vidole kuhusu Hong Kong
Wema mambo bado magumu, aachiwa, akamatwa tena