Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Kijana mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Mohamed Msangi (28) mkazi wa Kilakala Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kujipatia mkopo wa milioni 15 katika taasisi ya mfuko wa Rais Kanda ya Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa jambo hilo na kusema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa na askari walifuatilia na kumkamata mtuhumiwa huyo.

Aidha, Kamanda Mtei amesema kuwa baada ya kijana huyo kuhojiwa alikiri kufanya kosa hilo kwa kuomba mkopo katika taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Vilevile Matei amedai kuwa kijana huyo alipoomba mkopo huo aliorodhesha majina ya vijana wengine wanne akijifanya kuwa vijana hao wamejiunga kwenye kikundi hicho kisha kupatiwa mkopo huku hao vijana aliowaorodhesha wakiwa hawana taarifa yoyote.

“Tuache huu wizi kwa kutumia vyombo vinavyotoa mikopo kwani mikopo hii imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watu wa chini na hilo ndiyo lengo la Serikali kuwaondolea watu umasikini ili waweze kufungua viwanda vidogo vidogo na kujipatia kipato, lakini wapo watu wanatumia vibaya vikundi hivi,”amesema Kamanda Mtei

Video: Makamba, Dkt. Tulia, Polepole wamlilia mke wa Naibu Waziri Kangi Lugola
Tanzia: Mke wa Kingunge Ngombale Mwiru afariki dunia