Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini England pamoja na klabu ya Man Utd, Ashley Simon Young, anatarajia kuukosa mchezo wa hii leo, ambapo kikosi cha Louis Van Gaal, kitakua na shughuli ya kupambana na CSKA Moscow huko nchini Urusi.

Meneja wa Man Utd Laouis Van Gaal amesema, Ashley Young hatokua sehemu ya kikosi chake hii leo kutokana na kuendelea kusumbuliwa na maumivu wa kiazi cha mguu.

Mwishoni mwa juma lililopita, mshambulkiaji huyo mwenye umri wa miaka 30, alikosa mchezo wa ligi ya nchini England, dhidi ya Everton ambao walikubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri.

Wengine watakao kosekana kwenye mchezo wa hii leo, ni beki wa pembeni Luke Shaw ambaye anaendelea kuuguza jeraha la mguu wake wa kulia, Paddy McNair pamoja na James Wilson.

Mlinda mlango kutoka nchini Argentina Sergio Romero pamoja na mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Ecuador, Antonio Valencia, wamesafiri na kikosi cha Man utd kuelekea nchini Urusi, baada ya kukosekana mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo dhidi ya Everton.

Kuelekea katika mchezo huo, Van Gaal, amejinasibu kuwa katika maandalizi mazuri dhidi ya kikosi chake na amesisitiza kuhitaji kuona ushindi unapatikana ugenini.

Amesema mchezo wa hii leo una umuhimu mkubwa kama ilivyo michezo mingine, na ameahidi kutokumpumzisha mchezaji wake yoyote mwenye sifa ya kucheza, kwa lengo la kuhofia mpambano wa mwishoni mwa juma hili ambapo mashetani wekundu watakuwa wenyeji wa Man City kwenye uwanja wa Old Trafford.

Anna Mghwira ampiga kikumbo Magufuli
Msigwa Aeleza Kwanini Anamuunga Mkono Lowassa Wakati Alisema Wanaofanya Hivyo Wapimwe