Sherehe ya Harusi ni siku moja tu, na Ndoa ni ya maisha yote.

Mwanaume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya Ndoa.

Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.

Ukitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote.

Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.

Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa au kuolewa na mtu asiye sahihi.

Kuna iana tatu za wanaume wa kuwaepuka : walevi, wazinzi na wagomvi.

Kuna aina nne za wanawake wa kuwaepuka: wazinzi, wachawi, wagomvi na wasio tii.

Kuolewa na mchekeshaji haitakufanya uwe na ndoa yenye furaha.

Maneno matatu yanayojenga amani katika ndoa: Nakupenda, Samahani, na Asante.

Mafanikio ya ndoa siku zote ni pembe tatu: Mungu mmoja, Mume mmpja na mke mmoja.

Usioe/kuolewa na pesa au mali. Oa/olewa na mtu kwani pesa/mali hufilisika lakini utu hudumu milele.

Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko ndoa isiyo na amani.

Usiweke Kipaumbele chako kwa muonekanao mzuri wa mwanamke . Hakuna mwanamke mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa.

Ukiwa rafiki mwema, utawavuta marafiki wema. Vivyo hivyo kwa marafiki wabaya.

Asili ya mikono inayo jali ni moyo unaojali.

 

JPM Awaonya wachochezi Magazetini
Mzee Majuto adai kifo ndio kitamtenganisha na uigizaji

Comments

comments