Takribani siku 10 tangu Rais John Magufuli alipoamua kumuondoa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga baada ya kubainika kuwa aliingia bungeni na kujibu swali la Wizara yake akiwa amelewa, watu wake wa karibu wameeleza maisha yake yalivyo.

Akiongea kwa masharti ya kutotajwa jina, mtu wa karibu wa mwanasiasa huyo ameeleza kuwa hivi sasa mwanasiasa huyo ameshindwa kufanya kazi yoyote kwakuwa mwili wake umeendelea kutawaliwa na mshangao alioupata kwani hakuwahi kufikiria kuwa pamoja na urafiki mkubwa aliokuwa nao na Rais Magufuli angetumbuliwa.

“Kitwanga alitarajiwa asingetumbuliwa kwa mtindo ule. Rais Magufuli baada ya kujiridhisha kuwa alikuwa amelewa bungeni, hakumpigia hata simu. Alimtumbua juu kwa juu, yeye alifikishiwa taarifa tu,” chanzo hicho kinakaririwa na gazeti la Jambo Leo.

“Ndio maana hadi leo Kitwanga haamini. Sisi huwa tunazungumza naye, ameshindwa kabisa kufanya kazi yoyote. Ni kama mwili wake wote umekuwa wa baridi. Binafsi namhurumia, wengi tunamhurumia, ila wengi wetu imetutia woga, maana hakuna anayejiona salama,” kiliongeza.

Ilielezwa kuwa baada ya uamuzi huo wa Rais dhidi ya Kitwanga ambaye alikuwa anaandamwa na kuhusishwa katika mkataba tata kati ya Jeshi la Polisi na Lugumi, hakuna waziri ambaye anajiona salama tena kwani ni yeye pekee alikuwa anaonekana kuwa salama mikononi mwa mtumbuaji majipu (Rais Magufuli).

Usalama aliokuwa akiuwaza Kitwanga ulitokana na ukweli kuwa Rais Magufuli alikuwa rafiki yake wa karibu na aliwahi kutamka hadharani wakati akimuombea kura katika jimbo la Misungwi kuwa anampenda sana.

 

 

Chris Brown amchapa Shavu Wizkid
Nape: Kuna mambo najifunza kwa Lowassa