Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP. Muliro Jumanne amewatunuku vyeti vya pongezi Askari Polisi 78 wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa utendaji kazi bora wa majumu yao katika kuzuia vitendo vya kihalifu mwaka 2022.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo Januari 21, 2023 jijini Dar es Salam, Muliro amesema kwa mwaka 2022 Dar es Salaam ilikuwa na changamoto za vitendo vya kihalifu, lakini askari na maofisa walifanya kazi ya ziada ya kuzima na kuzuia vitendo vya kiuhalifu.

Askari wa Jeshgi la Polisi wakiwa katika majukumu yao ya ulinzi na usalama.

Amesema, Askari wote wamefanya vizuri ila waliopewa zawadi ni wawakilishi kutoka kila eneo la utendaji kazi kwa kujituma kwa kushirikiana na Askari wenzao na Wananchi, katika kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa salama mwaka 2022.

Aidha, Muliro amebainisha kuwa vigezo vilivyotumia kuwapata askari hao ni pamoja na nidhamu, weledi, uadilifu, ujasiri, kujituma, na utoaji huduma bora kwa wateja.

Wagombea urais washutumiana kwa ufisadi
Waziri afariki ghafla akiwa kwenye kikao