Jeshi la Polisi katika Kaunti ya Busia nchini Kenya linamshikilia askari magereza kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa mwenye virusi vya corona (covid-19) aliyekuwa katika eneo maalum lililotengwa na Serikali kwa ajili ya waathirika wa virusi hivyo.

Ripoti ya Polisi ambayo imeshuhudiwa na Citizen TV ya nchini humo, imeeleza kuwa askari mmoja aliyekuwa analinda katika eneo hilo usiku alianza kumuona askari mwenzake akiwa anamshawishi mgonjwa huyo kimahaba, alirejea katika chumba wanachokaa walinzi wenzake na kuwasilimulia alichokiona.

Hata hivyo, baada ya wenzake kuamua kwenda kumfuatilia askari huyo, hawakuwakuta yeye na mgonjwa [katika eneo alilokuwa amembananisha mgonjwa]. Ghafla, alianza kusikia kelele zikitoka katika wodi ya wanawake.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa baada ya maafisa hao wa polisi kukimbilia eneo hilo waliwakuta wagonjwa wakiwa nje, na walieleza kuwa askari magereza alikuwa anambaka mgonjwa mmoja wa kike.

Maafisa wa afya wa eneo hilo walifika katika eneo la tukio. Maafisa magereza waandamizi waliokuwa katika eneo hilo walimnyang’anya silaha mtuhumiwa na kumuweka karantini katika eneo hilo, akisubiri kuchukuliwa na jeshi la polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Kenye imethibitisha kuwa na visa 12,062 vya corona, wagonjwa 3,983 wamepona na 222 wamepoteza maisha.

Wateule wapya wa Magufuli leo, RC, DC…

Waziri Mkuu ahimiza viongozi wa dini kulinda amani

Trump ‘apiga chini’ sheria ya kuvaa barakoa
Wateule wapya wa Magufuli leo, RC, DC...