Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Koplo Daniel Warioba (43), kutoka Kikosi cha 92 TJ, kwa tuhuma za kumuua mke wake Joyce Ismail (35), ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Ruvu Darajani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa ameeeleza kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Desemba 4, katika eneo la Janga, Wilaya ya Kipolisi Mlandizi.

Kwa mujibu wa kamanda Wankyo, askari huyo anadaiwa kumchoma mke wake na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia kifo ambapo baada ya kutekeleza mauaji hayo, inadaiwa mtuhumiwa alitaka kunywa sumu kwa lengo la kujiua.

Wankyo amesema polisi wamemkamata mtuhumiwa huyo, na anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Tumbi, huku chanzo cha tukio hilo kikiendelea kuchunguzwa.

Mapigano yakwamisha misaada Tigray
COSTECH kutoa ruzuku kwa wabunifu na watafiti