Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ametoa zawadi ya fedha na hati ya ujasiri kwa maaskari 11 waliofanya vizuri katika tukio lililotokea Agosti 25, 2021 la kupambana na Hamza aliyezua taharuki katika barabara ya Ali Hassn Mwinyi karibu na zilipo ofisi za ubalozi wa Ufaransa Dar es Salaam.

Akiwa anawakabidhi hati hizo kwa niaba ya IGP Sirro leo Septemba 20, 2021 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa Polisi hao walifanya kazi kubwa na kufanikiwa kukomboa silaha mbili zilizokuwa na magazine mbili.

“Askari hawa Waliopambana na Hamza miongoni mwao walikuwa ni Askari 11, ambao kwa mamlaka za kisheria za uendeshaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP amewapa zawadi ya vyeti vya ujasiri na zawadi ya pesa kwa kadri alivyoona inafaa,” amesema Kamanda Muliro.

Muliro amesema Polisi walipambana kuhakikisha madhara makubwa hayatokei kwa sababu hakuna mtu angeweza kufahamu kama Hamza angeondoka na silaha zilizokuwa na magazine mbili na risasi 60 na nyingine alizokuwa nazo.

Aidha amesema kazi ya Polisi siyo ya kubezwa kama baadhi ya watu wanavyofanya, ameeleza kuwa polisi hulinda watu na mali zao ikiwa sehemu moja watu wanapiga risasi askari akaamua kufa kwaajli ya watu wengine sio kazi ya kubeza.

“Ninaendelee kuwa tia moyo Askari waliojeruhiwa kwenye mapambano kati ya polisi na Hamza na niendelee kuzitia moyo familia zilizopoteza wapendwa wao,” Amesema Muliro.

Manny Pacquiao atangaza kugombea Urais
Kaze atajwa tena Young Africans