Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, waliotimiza miaka 22 wakiwa kazini wametoa msaada katika kituo cha faraja Orphanage kilichopo shangalai wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha, ambacho kinalea watoto yatima na wahitaji.

Akiongea kwa niaba ya Askari wenzake, mara baada ya kutoa msaada huo, Sajenti Mwanema amesema wameona ni vyema kutoa msaada huo na kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda kwa kipindi hicho wakiwa kazini.

Aidha, amebainisha kuwa Askari Polisi hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa msaada kwa makundi yenye uhitaji, ambapo amewaomba watu wengine kutoa walicho nacho kwa watoto wenye uhitaji katika vituo vya watoto yatima.

Naye Mkurungenzi wa faraja orphanage, Mchungaji Faraja Malaki amewashukuru askari hao kwa mchango na msaada wao katika kituo hicho na kuwaomba wengine wenye moyo wa kujitoa wafike kituo cha faraja kusaidia watoto hao wenye uhitaji.

Akiongea kwa niaba ya watoto mara baada ya kupokea msada huo, Mtoto Jephason Faraja amewashukuru askari hao kwa kutoa msaada huo ambao umefanya wajisikie ni kundi linalokumbukwa katika Jamii.

Huduma bora kwa walemavu ni lazima: Serikali
Mtoto wa Museveni aibua utata mwingine