Askari wawili wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wameuawa kwa kupigwa risasi na watu ambao hawajajulikana, katika kijiji cha Msafiri wilaya ya Kibiti.

Watu hao pia walichoma moto gari moja na pikipiki moja zilizokuwa zikitumiwa na askari hao, na kisha kutokomea kusikojulikana.

Taarifa za tukio hilo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga ambaye alieleza kuwa anaendelea kufuatilia kwa kina.

Huu ni muendelezo wa matukio mabaya ya mauaji yanayolenga viongozi na askari katika maeneo hayo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro alitembelea mkoa huo na kukutana na wazee wa Kibiti. IGP Sirro aliwatumia salamu wanaoendesha mauaji hayo akiwataka kuacha mara moja.

Video: Bavicha wawaka kukamatwa Meya wa Ubungo
Video: Mkurugenzi Misungwi apewa masaa kutafuta ufumbuzi eneo la kujenga soko