Oparesheni ya kutumbua majipu iliyoasisiwa na Rais John Magufuli, limewagusa wengi na kuleta mtikisiko mkubwa kwa baadhi ya watendaji wa umma waliobainika kutumia ofisi zao vibaya.

Kilio cha mtikisiko huo kimemgusa Askofu Mkuu wa Kanisa la Good News For All Ministries, Charles Gadi aliyempigia magoti Rais Magufuli kuwaombea msamaha walisimamishwa kazi.

Askofu huyo ambaye amesema kuwa akiwa kama mtumishi wa Mungu anapaswa kuwaombea msamaha watu waliokosea, amemuomba Rais Magufuli awasamehe walimu wakuu na wakurugenzi waliofukuzwa kazi kwa kosa la kuchangisha michango mbalimbali katika shule za kata na kukiuka agizo la rais la ‘Elimu Bure’.

Kadhalika, Askofu huyo alimuomba Rais awasamehe watumishi 65 wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee waliokatika hatari ya kufukuzwa kazi kwa kosa la kukiuka agizo la Rais na kusafiri kwenda nje ya nchi bila kibali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Akofu huyo pia alimsifu Rais Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani ya kipindi cha muda mfupi na kuwataka watanzania wote kumuombea.

Chanzo: Nipashe

Kikosi Cha Mbeya City Kunolewa Na Phiri
Lowassa aweka mezani walichozungumza na Waziri Mkuu Majaliwa