Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (K.K.K.T) nchini Tanzania, Askofu Benson Bagonza amesema kuwa suala la amani siyo la wanasiasa peke yao na kuwa linapaswa kuhubiriwa na wadau wote ikiwa ni pamoja na taasisi za dini.

Amesema kuwa huwezi kuwazuia viongozi wa dini wasishiriki katika suala zima la siasa kwani kila kitu kinachofanyika kinatokana na siasa.

Askofu Bagonza ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ambao uliwahusisha pia viongozi wa dini.

“Viongozi wa dini wana wajibu wa kushauri na kuonya pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani, hivyo kujitenganisha dini na siasa haitawezekana,” amesema Askofu Bagonza

Hata hivyo, ameongeza kuwa maendeleo bila siasa hayawezi kuwepo, hivyo ni bora kukawa na uwanda mkubwa wa kushindana kwa hoja na uhuru zaidi.

Video: Hawa ni watu kumi hatari kwa usalama wa taifa letu- Musiba
Korea Kaskazini yaikaribisha Marekani mezani