Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekanusha madai kuwa amelishwa sumu kutokana na msimamo wake kuhusu chanjo.

Askofu Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, ameyasema hayo wakati wa ibada kanisani kwake. Amesema kuna watu wanataka kuwasingizia watu wengine au Serikali kupitia tuhuma hizo kuwa amenyweshwa sumu.

“Niwahakikishie kwamba hakuna serikali imemnywesha sumu Gwajima kwa kuwa serikali ndiyo inasema chanjo ni hiari. Hakuna wa kuninywesha sumu na hatotokea,” amesema Gwajima.

Kiongozi huyo pia alizungumzia suala la chanjo huku akisema suala la afya ya mtu linapaswa kulindwa na mtu mwenyewe.

Akijibu madai juu ya cheti kilichokuwa kikisambazwa mtandaoni kuonyesha kuwa Askofu huyo ameshapata chanjo hivyo anawadanganya Watanzania, amesema kwamba cheti kile ni cha kufoji na hata aliyefoji ni dhahiri kuwa hajui Kiingereza kwani badala ya kuandika ‘certificate’ ameandika ‘certicate’.

Aidha, Gwajima amesisitiza kuwa kila mwanachi anao wajibu wa kulinda afya yake na kusema kuwa yeye kama mpiga filimbi wa Tanzania atawalinda kondoo wake.

Kenya, Somalia kurejesha tena uhususiano wa kidiplomasia
Waziri Mulamula amuaga Balozi wa Oman