Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesema ameanza mchakato wa kununua Treni ya mwendo kasi ambayo itakuwa inatoka Dar es salaam mpaka Morogoro.
Amesema kuwa Tanzania ya Viwanda, haitoweza kufanikiwa kama hakutakuwa na usafiri wa uhakika wa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Aidha, Gwajima amesema kuwa teyari amefanikisha mpango wake wa kujenga Chuo cha Mafunzo ya kurusha ndege  na anasubiri ruhusa ya Rais Magufuli ili aanze shughuli nzima za ufundishaji.
”Naomba Serikali isiingize masuala ya siasa katika hili kwani lina manufaa kwa Watanzania wote, nimeamua kuwekeza ili kuwakomboa watanzania na kuzalisha ajira,”amesema Gwajima.
Hata hivyo, amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kushikamana katiak suala zima la maendeleo ili kuweza kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda..

Zitto: Msimamo wa Ndugai umetuokoa wabunge
Selasini naye ang'aka kuhusu Makonda