Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe amedai kuwa kuvuja kwa video ya Askofu Gwajima kumetokana na kurudisha uhusiano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Gwajima kwani wapo watu waliochukizwa kurejea kwa uhusiano huo.

Akizungumza kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo jijini Dar es Salaam, jana 12 Mei 2019, Askofu Kakobe amemtetea Gwajima kwamba, anachafuliwa kwa makusudi.

Akihubiri kanisani kwake, Kakobe amesema hawawezi kumtenga Gwajima wala Makonda kwa mapungufu walionayo.

“Hatuwezi kuwatenga wale mnaofikiri wana dhambi, na sisi kama wazee, kama Makonda ana upungufu, sisi si wanasiasa ni watumishi wa Mungu, tukimtenga tutamsaidiaje?” amehoji.

Aidha, Askofu Kakobe amewataka watu wenye ushahidi wa moja kwa moja ya kwamba, Askofu Gwajima alihusika katika video hiyo ajitokeze hadharani, na kama hayupo basi watu waache kumtuhumu kiongozi huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Askofu Kakobe amewataka waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kupuuza tuhuma hizo “wakati wa kila uongo kufanya kazi peke ake umepita, wakati huu ukimgusa mmoja umegusa wote ukimshambulia mmoja umegusa wote.

“Kwa hiyo wamegusa moto. Waumini msitange tange, usitafute kuja kwangu wala kwa yeyote hapa uko mahala salama,” amesema Askofu Kakobe.

Usafiri wa ndege waendelea kutia wasiwasi
Kodak Black afungwa jela ya kijasusi

Comments

comments