Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Tanga Anthony Banza amefariki Dunia jana Asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) ambako alikuwa anapatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa koo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TECP), Padre Charles Kitima kwenda kwa Mwadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofu Wakuu, Maaskofu wote, Watawa wa kike na wa kiume na na waamini wote imeeleza kuwa imeeleza kuwa tarehe ya mazishi itatangazwa baadaye.

“Kanisa linatoa pole kwa familia yote ya jimboni Tanga na KanisaKatoliki Tanzania kwa ujumla kwa msiba huu mkubwa, Baraza linamuombea kwa Mungu marehemu Baba Askofu Banzi, roho yake ipumzike kwa amani Mbinguni pamoja na watakatifu,” imeeleza taarifa hiyo.

Mbali na kuwa Askofu wa jimbo la Tanga, Banzi amewahi kuwa Mwenyekiti na Mlezi wa mashirika ya masista na watawa wote Tanzania.

Askofu Banzi amefariki akiwa na umri wa miaka 74 naSeptemba 15 mwaka jana alitimiza miaka 25 tangu kuwekwa wakfu kuwa Askofu katika sherehe ya Jubilei iliyofanyika jimboni Tanga.

Katibu Mkuu: Mkitoa majoho hapa ni aibu
Serikali yapunguza msongamano wa wafungwa magerezani